Luke 24:1-6

Kufufuka Kwa Isa

(Mathayo 28:1-10; Marko 16:1-8; Yohana 20:1-10)

1 aMnamo siku ya kwanza ya juma, alfajiri na mapema, wale wanawake walichukua yale manukato waliyokuwa wameyaandaa, wakaenda kaburini. 2 bWakakuta lile jiwe limevingirishwa kutoka kwenye kaburi, 3 clakini walipoingia ndani, hawakuuona mwili wa Bwana Isa. 4 dWalipokuwa wanashangaa juu ya jambo hili, ghafula watu wawili waliokuwa wamevaa mavazi yanayong’aa kama umeme wakasimama karibu nao. 5Wale wanawake, wakiwa na hofu, wakainamisha nyuso zao mpaka chini. Lakini wale watu wakawaambia, “Kwa nini mnamtafuta aliye hai miongoni mwa wafu? 6 eHayuko hapa; amefufuka! Kumbukeni alivyowaambia alipokuwa bado yuko pamoja nanyi huko Galilaya kwamba:
Copyright information for SwhKC